Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam watakiwa kuendelea kuchukua hatua za tahadhari ili kujikinga maabukizi dhidi ya virisi vya corona.

Hayo yamesemwa na mganga mkuu wa mkoa huo Dkt. Rashid Mfaume wakati akipokea msaada wa barakoa 17500 na lita 700 za vitakasa mikono kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali la Mediapiace linalohusika na mradi wa mama na mtoto katika mkoa wa Dar es Salaam.

Dk Mfaume amesema kuwa msaada huo utaelekezwa katika hospitali ya sinza, Vijibweni, Rangitatu, vituo vya afya vya kimara, Tandale, Mbezi na zahanati za Tegeta na Bunju.

Ameongeza kuwa licha ya elimu inayotolewa na wataalamu wa Afya ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona, shirika hilo linawahamasisha wananchi wasibweteke katika kipindi hiki ili kuutokomeza ugonjwa huo nchini.

Naye mwakilishi wa shirika hilo Sukyung Kim amesema limekuwa likishirikiana na wizara ya Afya na TAMISEMI katika kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto.

Uganda: maambukizi yafikia 274 visa 10 vyaongezeka
Oxfam kufunga ofisi zake nchi 18 Tanzania yatajwa

Comments

comments