Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amesema tayari mtambo wa pili katika bwawa kubwa lenye utata kwenye mto Blue Nile umeanza kuzalisha umeme, licha ya pingamizi zinazoendelea toka nchi za Misri na Sudan kuhusu mradi huo.

Cairo na Khartoum zinahofia kwamba huenda Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD), linaweza kutishia upatikanaji wao wa maji muhimu ya Nile, na kudai makubaliano ya maandishi juu ya uendeshaji wa bwawa hilo.

Mapema mwezi Julai 2022, Misri iliandikia barua kwa Baraza la Usalama la Kimataifa, ikitoa pingamizi lake kwa mipango ya Ethiopia juu ya mradi wa umeme wa bwawa hilo kwa mwaka wa tatu bila makubaliano ya pande tatu.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed akiongelea juu ya mradi huo wa umeme mbele ya vyombo vya Habari.

Msemaji wa Mambo ya Nje Meles Alem amesema, “Kumekuwa na taarifa kwamba mafuriko yametokea katika miji ya Misri na Sudan, hii inaonyesha kuwa ujenzi wa Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance hautawadhuru wananchi wa Misri na Sudan, wakati ujenzi ukiendelea.”

Msemaji huyo, pia alithibitisha kuwa Wanajeshi wanashiriki kikamilifu kuwafukuza kundi la al-Shabaab hadi kwenye mpaka na Somalia ili kulinda eneo hilo na kudai kuwa, “Al-Shabaab ni tishio la usalama kwa ulimwengu na kanda. Maadamu al-Shabaab ni tishio la usalama, tutafanya operesheni muhimu za usalama nchini Ethiopia,” amesema.

Ethiopia, ilianza kuzalisha umeme katika bwawa hilo Februari 2022, ambapo hivi sasa, mitambo hiyo miwili, kati ya 13 inayotrajiwa kujengwa kwenye bwawa hilo, na itazalisha megawati 750 za umeme huku GERD ikitarajiwa kuzalisha zaidi ya megawati 5,000, mara mbili ya pato la sasa la Ethiopia.

Tahadhari yatolewa uwepo wa mapigano karibu na Nyuklia
Iringa kupokea ndege za abiria zaidi ya 70