Mshukiwa wa kwanza wa mauaji ya rapa kutoka nchini Marekani Young Dolph, ametambulika baada ya gari lililohusika kuwabeba watu wawili waliofanya mauaji ya rapa huyo kukutwa katika eneo ambalo liliwapa wachunguzi dalili za moja kwa moja zilizohitajika ili kumuunganisha na kesi hiyo.

Polisi walimtangaza Jumatano kijana aitwaye Justin Johnson mwenye umri wa miaka 23 kuwa anatafutwa na jeshi hilo akihusishwa na kesi ya mauaji Dolph.

Johnson ni rapa chipukizi wa eneo la Memphis nchini Marekani ambaye anafahamika kwa jina la Straight Drop ambapo moja ya vielelezo vilivyomuhusisha na kesi hiyo ni baada kubainika kuwa eneo lilipokutwa gari lililokuwa limewabeba wauaji ni moja ya maeneo aliyowahi kuyatumia kwenye video zake kadhaa za muziki.

Imetajwa video ya wimbo wake ‘Going Straight In’ aliyoitoa mnamo Novemba 21, 2021. Video iliyowahusisha watu wengi nyuma yake.

Muda mfupi baada ya Dolph kuuawa, wapelelezi walilifuatilia gari lililowabeba wauaji hao waliotoroka muda mufupi baada ya kumuua Dolph wakitumia gari aina ya Mercedes nyeupe.

Baada ya kufuatilia kwa muda walilikuta gari hilo likiwa limetelekezwa nje ya nyumbani sawa na iliyoonekana kwenye video ya Johnson huko Memphis Marekani.

Johnson yuko kwenye orodha ya orodha ya wanaotafutwa na jeshi la upelelezi la Marekani FBI, kwa kuhusishwa  na uhalifu uliopangwa na anapaswa kuwekwa kizuizini kwa kesi ya mauaji na kumiliki silaha hatari.

Polisi wameahidi zawadi ya $15,000 sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 346 za Kitanzania kwa atakayefanikisha kukamatwa kwake.

Dolph aliuawa Novemba 17, ambapo video ya muziki iliyoshukiwa na jeshi la polisi nchini humo ilitoka na kuwekwa kwenye mtandao wa YouTube Novemba 21, 2021 muda mfupi tu, baada  ya kuuawa kwa kupigwa risasi.

BMW wazindua gari inayoweza kujibadilisha rangi
Nadia Mukami amjibu Jalango, ujauzito wa siri