Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro leo amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha.

Waziri Ndumbaro ametoa maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema uchunguzi huo hauhusiani na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Nafasi ya Mdachi itakaimiwa na Betrita James ambaye ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi TANAPA, hatuwezi kumchunguza Mtu akiwa kakalia kiti hichohicho” amesema Ndumbaro.

Uchaguzi Buhigwe, Muhambwe kufanyika Mei 16
Mama mzazi wa IGP Sirro afariki dunia