Meneja wa Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard Kanda ya Ziwa, Captain Manika Kihiri amesema wamemuondoa katika eneo la hospitali mlinzi aliyemshambulia Daudi Lefi aliyekuwa akimuuguza mgonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, hii ikiwa nia hatua ya awali waliyochukua.

Kihiri amesema kinachofuata watatekeleza maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kinidhamu akibainisha kuwa Suma JKT haipo kwa ajili ya kuzua taharuki bali kuleta amani.

Tukio hilo limetokea Ijumaa Januari 22, 2021 saa 11 jioni ambapo Daudi Lefi (45), akiwa katika wodi ya wanawake namba 1 ambako Mama yake mzazi Victoria Lugano Mwakagari amelazwa, alishambuliwa kwa kupigwa kwa mkanda sehemu mbalimbali za mwili wake na Mlinzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard, Geofrey Paul akimtaka aondoke wodini kwa kuwa muda wa kusalimia wagonjwa umeisha.

Meneja Tanesco atakiwa kujibu sababu kukatika kwa umeme
PICHA: Mkuu wa JKT akagua ujenzi skimu ya umwagiliaji