Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), John Mnyika amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuweza kuamua kujenga barabara ya njia nane.

Amesema kuwa Watanzania wamemuombea asiwe na kiburi, huku akisema Wananchi wana malalamiko juu ya Bomoabomoa ambapo amemuomba kutanguliza utu, wa Mwl. Nyerere mbele.

Aidha, Mnyika ameongeza kuwa maendeleo ni ya vitu lakini maendeleo zaidi ni ya watu huku akimtaka atafakari kuwalipia fidia Wananchi waliopisha ujenzi huu.

”Demokrasia na Maendeleo ni mapacha, tunakuomba Rais unapofanya kazi za Miradi ya Maendeleo vilevile ukatumia fursa hii kuzungumzia kuondoa vikwazo vinavyoikabili Demokrasia ya Nchi ambayo tunaamini vitasaidia Nchi kusonga mbele,”amesema Mnyika

Pia ameongeza kuwa kuna mambo matano yanatoka kwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambayo anawaomba Watanzania na Rais kwa ujumla kuweza kuyatafakari kwa muda huu tunapoelekea mwaka 2019.

Hata hivyo, Mnyika amesema kuwa akisikia Wafanyakazi wa Umma wanalilia kikokotoo, wengine wamepandishwa madaraja hawajapandishwa mishahara, Wafanyabiashara wanalia Mtaani, na kumuomba akipata nafasi ya kuzungumza pamoja na uzinduzi utatoa matumaini ya Taifa kwa 2019 na 2020″

Ujumbe wa Dogo Janja waibua maswali
Jumuiya ya wazazi CCM yampongeza mbunge Neema Mgaya

Comments

comments