Meneja wa klabu ya Man Utd Jose Mourinho, anaamini kiasi cha fedha pesa kilichotumika katika usajili wa kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba kitarudi, huku akisisitiza nyota huyo ana miaka takriban kumi mbele ya kung’aa.

Pogba amekamilisha uhamisho wake wa Euro mililioni 110 kurudi Old Trafford akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Italia Jeventus FC mapema leo asubuhi.

“Ana nafasi ya kuwa moyoni mwa mashabiki wa klabu hii kwa miaka kumi na zadi,” Mourinho amesema

“Paul ni moja ya wachezaji bora duniani na atakuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha United na nataka nimfanye awe tegemeo kubwa kwa siku za usoni.”

“Ana kasi, nguvu, anafunga na ana uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo vizuri kuliko wachezaji wengi ambao wamemzidi umri.”

“Kwa umri wake wa miaka 23, ana nafasi ya kujimilikisha nafasi yake kwa miaka mingi zaidi. Bado ni kijana ataendelea kuimarika zaidi.”

Pogba amedumu Juventus FC kwa miaka minne, ameshinda ubingwa wa Serie A kwa miaka yote minne. Mourinho anaamini Mfaransa huyo atahamishia makali yake kunako Old Trafford na kurejesha heshima ya Man United iliyopotea kwa tangu msimu wa 2012-13.

Makonda Ashambuliwa Na Wanajangwani
Dk. Kigwangallah akana uhusiano na ‘Dk Mwaka’