Meneja wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho amemjibu mchezaji wa zamani wa Arsenal Paul Merson, ambaye alisema mreno huyo amekua sababu ya kuharibu vipaji vya wachezaji.

Mourinho amejibu tuhuma hizo, baada ya kikosi cha Spurs kuambulia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Manchester United mwishoni mwa juma lililopita, ambapo mshambuliaji Harry Kane hakuonyesha makali yake kama alivyokuwa chini ya meneja Mauricio Pochettino.

Katika mchezo huo Kane aligusa mipira mara 36 tu na kufanikiwa kupiga shuti moja lililolenga lango la wapinzani, mlinda mlango Hugo Lloris ndiye aliyegusa mara chache zaidi ya mshambuliaji huyo kutoka England, ambaye tayari ameshazifumania nyavu mara 11 msimu huu.

“Nafikiri Kane hana shida ya kufunga kwenye kiosi change, hasa anapokuwa fiti asilimia 100” alisema Jose Mourinho.

“Ulikuwa mchezo ambao Manchester United walipata nafasi nyingi, ndiyo maana mshambuliaji wao Anthony Martial alipata nafasi, lakini Kane angepata zile angefunga bila shida” aliongeza kocha huyo mwenye maneno mengi.

Wakati akitetea tuhuma za kuwaharibu washambuliaji, kocha Jose Mourinho ametaja orodha ya washambuliaji ambao alifanya nao kazi na wakatwaa viatu vya dhahabu vya ufungaji bora kama Didier Drogba, Cristiano Ronaldo, na Zlatan Ibrahimovic ambaye alifanya nae kazi Manchester United na Inter Milan.

“Nina idadi nzuri ya washambuliaji ambao walifanya kazi nzuri chini yangu” alisema.

Azam FC yawasili Kagera
‘Mlitaka nife?’, Vanessa afunguka ‘mauzauza’ aliyokutana nayo kwenye muziki