Mtoto wa Rais wa Uganda, Jenerali Muhozi Kainerugaba kwa mara nyingine ameibua mjadala kupitia ukurasa wake wa wa mtandao wa kijamii wa Twitter, baada ya kutuma ujumbe wenye utata aliouambatanisha na picha ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Jenerali Kainerugaba katika ukurasa wake ameandika kuwa, ‘’Mimi ni Jenerali wa nyota 4 wa UPDF (Jeshi la Uganda), kuna vitu vichache ambavyo sijaviona katika dunia hii. Lakini ninawahurumia wale wanaomdharau mjomba wangu, Jenerali Kagame. Kupigana na Rwanda inamaanisha kupigana na Uganda!

Tweet ya Mtoto wa Rais Museveni, Muhoozi Kainerugaba.

Kauli ya Muhooozi inakuja wakati ambao mzozo kuhusu wapiganaji wa kundi la M23 na Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na Rwanda na Congo inaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23 walioteka maeneo mashariki mwa nchi hiyo, madai ambayo Rwanda inayakanusha.

Kwa upande mwingine inaishutumu DRC kwa kushindwa kutimiza ahadi ya kuwarejesha nyumbani waasi wa Rwanda wa kundi la FDLR walioko mashariki mwa DRC inaowashutumu kuhatarisha usalama wa Rwanda, ambapo hivi karibuni pande mbili zilirushiana maneno, kila upande ukielezea uwezekano wa kuingia vitani iwapo usalama wake utayumbishwa.

Askari waliotimiza miaka 22 kazini watoa msaada
Katavi wavuka lengo utekelezaji afua za UKIMWI