Jaber al-Bakr, aliyekuwa anatuhumiwa kwa kupanga shambulizi la bomu ameripotiwa kujiua akiwa katika chumba cha mahabusu, Leipzig nchini Ujerumani.

akabar

Jaber al-Bakr (22)

Maafisa wa Ujerumani wamesema kuwa mtuhumiwa huyo raia wa Syria alijisalimisha polisi Jumatatu ya wiki hii kufuatia msako mkali dhidi yake na kwamba tangu alipowekwa mahabusu alianzisha mgomo wa kula chakula.

Kwa mujibu wa BBC, Kitengo cha Intelijensia cha Ujerumani kilieleza kuwa kilipokea taarifa wiki iliyopita kuwa al-Bakr angeweza kuandaa shambulizi la kigaidi.

Imeelezwa kuwa baada ya kumfuatilia kwa ukaribu, waligundua wiki hiyo iliyopita kuwa alitumia mtandao kutafuta maelekezo ya namna ya kutengeneza bomu na kwamba walikuwa na vilipuzi.

Mdee, Kubenea waanza kuonja joto la Mahakama kwa kumpiga Katibu Tawala
VIDEO: YCEE AUNGANA NA DJ MAPHORISA KUTENGENEZA REMIX KALI YA ‘O’MO ALHAJI