Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Chriss Mugalu, amerudi nchini kwao DR Congo kwa ajili ya kujiuguza.

Mugalu alipata majeraha wakati Simba SC ikiwa kwenye maandalizi ya kucheza dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana mwezi uliopita.

Mshambuliaji huyo amesema amelazimika kurudi nyumbani kwao ili apate muda wa kupumzika na kuendelea na tiba.

“Bado sijafahamu naweza kurejea wakati gani uwanjani lakini matibabu ambayo nayafanya sasa ni hali ya juu na natakiwa kupumzika muda mwingi ndio maana nimerudi nyumbani,” amesema na kuongeza

“Nikiwa hapo Tanzania nikiona wachezaji wanzangu wanaenda mazoezini, kambini au uwanjani kucheza mechi huwa naumia mno jambo ambalo huenda lingefanya akili yangu kutokuwa sawa na kuchelewa kupona kwa haraka,”

“Nitarudi Tanzania baada ya maendeleo yangu kuwa vizuri na muda ambao nitatakiwa kufanya yale mazoezi madogo madogo kabla ya kujiunga na wenzangu.”

Mugalu alimaliza nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora msimu uliopita 2020/21, akitanguliwa na mshambuliaji mwenzake wa Simba SC John Bocco.

Wananchi 80,000 hadi 100,000 kuchanja kwa siku
Bosi wangu alivyonogewa na penzi langu