Hospitali ya Taifa Muhimbili inafanya upasuaji wa kihistoria wa kutenganisha watoto mapacha walioungana leo July 1, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa za hospitali hiyo, Upasuaji huo unaohusisha mapacha walioungana kifua, na sehemu ya ini ingawa kila mtoto ana ini lake itahusisha wataalam 31 wa matibabu na utafanyika kwa saa 7.

Timu hiyo ya madaktari 31 inajumuisha Watanzania 26 na wataalam 5 kutoka Ireland, akiwemo daktari mkuu wa upasuaji.

Upasuaji huo utakuwa wa kwanza wa aina yake nchini Tanzania, na wa tatu pekee kufanyika barani Afrika, huku upasuaji mwingine ukifanyika Afrika Kusini na Misri.

Upasuaji huo utagharimu takriban Shilingi milioni 50, ambapo ungefanyika nje ya nchi ungegharimu zaidi ya Shilingi milioni 120.

Upasuaji huu mkubwa na wa kihistoria umekuwa sehemu ya jitihada za serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikipunguza mzigo wa gharama kwa Watanzania kwa kumudu kufanya upasuaji nyumbani, tofauti na nje ya Tanzania ambako gharama ni kubwa zaidi.

Upasuaji wa kwanza wa mapacha walioungana ulifanyika nchini Tanzania mwaka 1994, lakini haukufaulu kwa sababu mtoto mmoja alifariki baada ya siku 63.

Taarifa zaidi kuhusu upasuaji huu endelea kuitembelea Dar24 Media.

Waziri Mkuu aachia madaraka
Uongozi Simba SC wamkingia kifua Barbara Gonzalez