Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema kuwa uongozi wa (MNH), utaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo na kushughulikia tatizo la upungufu wa wauguzi.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani, Tawi la Muhimbili ambayo huadhimishwa Mei 12 kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “ Wauguzi Mbiu ya Kufikia Malengo Endelevu ya Milenia.”
Aidha, akizungumza hospitalini hapo, amesema kuwa uongozi wa hospitali unashughulikia posho za wauguzi na pia kuboresha mazingira ya kazi ili wauguzi waweze kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
 
“Hii ni hospitali ya Taifa ambayo inategemewa na hospitali nyingine kujifunza mambo mbalimbali. hivyo nawapongeza wauguzi kwa kuandaa mada mbambali na kuziwasilisha kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani,” amesema Prof. Museru.
Hata hivyo, Katika kongamano hilo wauguzi na wataalamu wengine waliwasilisha mada mbalimbali kuhusu wanavyotoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa na jinsi ya kuboresha huduma kwa wagonjwa wa kansa, figo na kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa magonjwa ya  dharura na ajali.
 

Video: Tumekubaliana tumwache Meya akae polisi-Lema
Kesi ya Kitilya na wenzake yazidi kuota mbawa