Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, ametoa siku 15 kwa Kampuni ya Derm Electric Limited inayosimamia mradi wa umeme vijijini (REA II), kuwaunganishia umeme wananchi wote mkoani Mara,wanaohitaji nishati hiyo waliojiandikishwa katika mradi huo.

Ametoa agizo hilo wakati anahitimisha ziara yake ya kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme vijijini wa awamu ya pili wilayani Butiama.

“Meneja wa wilaya na mkandarasi mrudi hapa kwenye vijiji hivi vya Sirorisimba na Buswahili, nyinyi Tanesco mtoe elimu na wewe mkandarasi uendelee na shughuli yako ya kuhakikisha wote wanaohitaji huduma ambao wamo ndani ya mradi wanaunganishiwa ndani ya siku 15″amesema Muhongo.

Hata hivyo, Muhongo amepiga marufuku kwa mkandarasi huyo kuruhusiwa kufanya kazi nyingine ya mradi wa umeme vijijini hadi atakapo kamilisha zoezi la kuwaunganishia wananchi kwenye maeneo aliyopewa awali.

Dk. Mongela ahofia kasi ya JPM
Magufuli atangaza neema tena