Hatua ya serikali ya Uganda kutaka kubadilisha katiba ili iwe na nguvu za kumiliki ardhi mahali popote wakati wowote, imepata pigo mara baada ya wabunge wa chama tawala kukataa kumuunga mkono Rais Museveni.

Wabunge hao wamepinga hatua ya Rais huyo ya kutaka kubadili katiba ya nchi hiyo huku wakisema itasababisha matatizo makubwa nchini humo.

Aidha, wabunge 278 kutoka chama tawala cha national resistence movement NRM, wameikataa nia ya Serikali kutaka kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo katika mkutano ulioitishwa na Rais Museveni

Wamesema kuwa hakuna namna ya kuwashawishi raia wa nchi hiyo kukubali kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo ili kuiruhusu Serikali kumiliki ardhi kimabavu, wakati wowote mahali popote kwaajili ya kutekeleza miradi ya Serikali.

Hata hivyo, wabunge hao wamekubaliana kuunda kamati maalumu itakayokuwa ikishughulikia masuala ya ardhi kote nchini humo, endapo Serikali itahitaji kutekeleza miradi ya maendeleo mahali popote pale.

Kagame kuiongoza Rwanda kwa muhula mwingine tena
Kiongozi wa upinzani Zambia aachiliwa huru