Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma (MwanaFA), amekutana na Wakuu wote wa Idara na vitengo vya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, ili kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya utatuzi wa changamoto zinazojitokeza katika kuwatumikia wananchi.

Wakiongea katika kikao hicho, wote kwa pamoja walijadili namna ya kushughulikia changamoto hizo, ikiwa ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku yenye lengo la kufikia malengo waliyojiwekea.

Aidha, wakiwa katikati ya kikao hicho, walipata ugeni wa ghafla wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahman ambaye aliwasalimia na kuwasihi kuhakikisha wanatekeleza ilani ya Chama tawala inatekelezwa kwa ufanisi.

Wengine ni waliohudhuria Kikao hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri na Sektetarieti ya CCM ya Wilaya ikiongozwa na Katibu wa CCM Wilaya, Simon Leng’ese.

Young Africans yamkana Ulimwengu
Kocha Simba SC amkataa John Bocco