Mwanamke mwenye asili ya Tanzania, Tanzeela Qambrani ameweka historia ya kuwa Mbunge wa kwanza mwenye asili ya Afrika akiiwakilisha jamii ndogo iliyotengwa ya Sidi iliyoko katika eneo la Markan na Karachi

Mababu wa Mwanamke huyo walihamia nchini humo kama watumwa karne moja iliyopita. Jamii ya Sidi au Sheedi au Habashi ni ya wahamiaji kutoka nchi za Maziwa Makuu (Afrika Mashariki).

Aidha, Tanzeela alipendekezwa kuwania nafasi hiyo kutoka katika chama (Pakistan Peoples Party) kilichotoa Waziri Mkuu wa kwanza Mwanamke, Benazir Bhutto

Hata hivyo, Wakati akihojiwa Tanzeela alieleza kuwa anayofuraha kupata nafasi hiyo kwani ataleta uwakilishi wenye tija katika bunge la nchi hiyo.

Video: RC Mbeya afanya ziara ya kushtukiza shule ya msingi, ambana walimu mkuu
Chile, Peru wenyeji wa fainali za klabu Amerika kusini 2019