Maafisa wa Serikali wanaosimamia operesheni ya kuwatafuta manusura waliosalia ndani ya msitu wa Shakahola na ufukuaji wa makaburi walipata miili miwili na kumuokoa mtu mmoja ambaye alikuwa na hali mbaya, huku idadi ya waliofukuliwa ikifika watu 240.

Miili hiyo, ilichukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya kaunti ndogo ya Malindi, ambapo awamu ya pili ya kufanyia upasuaji maiti hizo kwa ajili ya uchunguzi, ikitarajia kuanza kazi hii leo Mei 25, 2023.

Zoezi hilo, litaongozwa na Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali, Dkt Johansen Oduor ambapo jumla ya maiti 128 zitafanyiwa upasuaji kufuatia zoezi la awali la miili 112 ambayo tayari ilishafanyiwa upasuaji kubaini kilichosababisha vifo vyao.

Maafisa hao pia wanasema mara baada ya kumuokoa mtu huyo mmoja sasa anafanya idadi ya waliokolewa kufikia watu 34 tangu kuanza kwa operesheni hiyo na idadi ya familia zinazotafuta jamaa zao waliopotea bado imesalia kuwa ni 613.

Hdi kufikia siku ya Jumanne wiki hii (Mei 23, 2023), tayari familia tano zilikuwa zimeshawatambua jamaa zao na kufikisha familia 19 zilizofaulu kutambua jamaa zao kupitia vipimo vya vinasaba – DNA.

Azam FC: Dakika 180, alama 06
Robertson azigonganisha Man City, Arsenal, Real Madrid