Katibu wa muungano wa wafanyazi nchini Kenya, COTU, Francis Atwoli amekerwa na maneno ya Naibu Rais, William Ruto, kuhusu vazi lake shingoni.

Atwoli alisema DP Ruto amekuwa akikosea heshima rosari ambayo yeye huivaa shingoni kama ishara ya dini yake na kusema ni nyororo anavalia shingoni licha ya umri wake.

Aliongea kuwa matamshi ya DP Ruto yatakuwa na mkosi kwake ikiwamo kupoteza kwenye uchaguzi wa urais katika uchaguzi mkuu ujao akidai kuwa Ruto amekuwa na mikosi mingine kama vile kufariki dunia kwa maaskofu ambao wamekuwa wakifuata DP ikiwa ishara ya hasira ya Mungu.

“Ananishambulia kwa sababu ya kuvalia rosari na kufikia sasa karibu maaskofu nane ambao walitaka kupata pesa kutoka kwake wamefariki. Hii inamaanisha yeye si mtu wa Mungu,” alisema Atwoli.

Alisema rosari huonyesha uaminifu wake kwa Muumba na hivyo Ruto alifanya kosa sana kusema ni nyororo na amekuwa na rosari hiyo kwa miaka kadhaa tangu abatizwe mwaka wa 1962 na Father John Kemba.

Wakati wa ziara yake eneo la Magharibi, DP Ruto akiongea eneo la bunge la Likuyani alisema Atwoli anavalia nyororo.

“Yule mzee wa nyororo alikuwa anasema ati mimi sitafika kwa debe …Sahi wameanza propaganda ingine ati ata huyu deputy president akishinda kura ‘Deep State’ na ‘system’ haiwezi kubali atangazwe kuwa president,” alisema.

Harakati za Uchaguzi Mkuu nchini Kenya zimekua zikiendelea ambapo vinara wa kila chama wamekua wakiendelea na kampeni zao kwa kuwekeana tambo za kila aina.

Treni yapinduka Tanga na kuua mtoto mmoja
Vinara uchaguzi Kenya waendelea kutambiana wakimtaja Rais Kenyatta.