Kocha Mkuu wa klabu ya Young Africans Nasreddine Mohamed Nabi tayari amekabidhi ripoti yake kwa viongozi wa klabu hiyo, ili kufanikisha mipango na mikakati ya kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika ripoti ya Kocha huyo kutoka nchini Tunisia inadaiwa ameutaka Uongozi kufanya usajili wa wachezaji wanane wa nguvu, ili kuendana na ushindani uliopo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) na michuano ya kimataifa msimu ujao.

Wachezaji wanaohitajika Young Africans kwa mujibu wa mapendekezo yaliyowasilishwa na Kocha Nabi kupitia ripoti yake ni Mlinda Mlango mmoja, Mabeki watatu (wa kulia, kushoto na Kati), Kiungo Mchambuliaji mmoja, Winga mmoja na Washambuliji wawili wa nguvu katika wachezaji hao Nabi anataka wachezaji watano wawe wa kimataifa huku watatu wazawa.

Pia Kocha huyo alietua klabuni hapo kuchuakua nafasi ya Cedric Kaze, amependekeza kuachwa kwa wachezaji wanne wa Kimataifa na wachezaji watano Wazawa, ili kupisha wale watakaosajiliwa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.

Uongozi wa Young Africans tayari umeshaanza kusajili, huku ukiripotiwa kumalizana na Beki wa Kulia wa Djuma Shaban raia wa DRC Congo na Sasa inafanya mazungumzo na wachezaji wengine ili kukamilisha usajili uliotajwa na kocha.

Kibu: Simu za viongozi Simba, Young Africans hazikauki
Mzee Matata wa Mizengwe afariki dunia