Klabu za ligi kuu ya soka Tanzania bara, zitakua zikilipwa shilingi milion 126, badala ya milion 100 kama malipo ya michezo yao kuonyeshwa moja kwa moja kwa njia ya televisheni na kampuni ya Azam Media Ltd.

Mabadiliko hayo ya malipo yamekuja baada ya kampuni ya Azam Media Ltd kuingia mkataba mpya wa miaka mitano na shirikisho la soka nchini TFF, ambalo lina haki zote za ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Mkataba huo wa kurusha matangazo Live ya Ligi Kuu Bara utagharimu Sh bilioni 23.

Katika mkataba uliosainiwa leo, kila klabu shiriki itapata Sh milioni 42 kwa mafungu matatu ambayo ni Sh milioni 126.

Fungu la mwisho la milioni 42 litatolewa kwa mfumo tofauti ambao utakuwa hivi.

Timu inayoshika nafasi ya juu katika msimamo inafaidika kwa kupata zaidi na itakwenda hivyo hadi chini.

Maana yake ligi itakapoisha, zitazokuwa juu kimsimamo zitapata fedha nyingi zaidi na zilizo chini zitaendelea kusota kwa kupata kiduchu.

Lengo kuu ni kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa kila kikosi kuona umuhimu wa kukaa juu katika msimamo wa ligi hali itakayochangia ushindani uwanjani kwa kila timu kutaka kushinda karibu kila mechi ili mwisho wa ligi ifaidike.

Rais Museven Azua Mjadala Mtandaoni
Rais Magufuli Awataka Wakurugenzi Kuwa Watatuzi wa Kero