Vituo 24 vya mitihani ambavyo ni sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote 17,935 vilivyofanya mtihani ambavyo vimethibitika kupanga na kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2022 vimefungiwa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani (NECTA), Athumani Amasi hii leo Desemba mosi, 2022 na kuongeza kuwa, NECTA imevifunga vituo hivyo hadi pale itakapojiridhisha kuwa vipo salama kwa shughuli za uendeshaji wa mitihani.

Vituo vilivyofungiwa na pamoja na Kazoba Primary – Karagwe, Mugini Primary iliyopo Magu Mwanza, Busara – Magu, Mwanza, Jamia Primary – Bukoba, Ukerewe Primary – Mwanza, Peaceland – Ukerewe, Karume Primary – Bukoba na Al Hikma Primary – Dar es salaam.

Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani (NECTA), Athumani Amasi.

Vituo vingine ni Kadama Primary – Chato), Rweikiza Primary – Bukoba, Kilimanjaro Primary -Arusha, Sahare Primary -Tanga, Winners Primary – Mwanza, Musabe Primary – Mwanza na St. Anne Marie Primary – Ubungo, Dar es salaam.

Aidha, vituo vingine vilivyofungiwa ni Leaders Primary -Rorya, Kivulini Primary – Mwanza, St Severin Primary – Biharamulo, Elisabene Primary – Tunduma, High Challenge Primary – Arusha, Tumaini Primary – Sengerema Mwanza, Holele Primary – Mwanza, Must Lead Primary – Chalinze na Moregas Primary -Tarime.

Kuona matokeo ya Darasa la saba mwaka 2022 yaliyotangazwa hii leo Desemba Mosi, 2022 bonyeza hapa https://necta.go.tz/psle2022/psle.htm

Wengi wanaishi na VVU bila kugundulika: WHO
Tazama matokeo darasa la saba, ufaulu wapanda