Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema kuwa Wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jurusalem ndio mji mkuu wa Israel ili amani iweze kupatikana.

Amesema kuwa Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa takribani miaka 3,000 na haujawahi kuwa mji mku wa watu wengine.

Aidha, ameyasema hayo huku kukiwa na maandamano makubwa yakiendelea kwenye ulimwengu wa kiislamu kufuatia hatua ya Marekani kuutambua Jurusalem kuwa ni mji mkuu wa Israel.

“Unaweza kusoma katika kitabu kizuri zaidi duniani, kinaitwa Biblia, Unaweza kusikia katika historia ya jamii wa wayahudi kote duniani, mji mkuu wa Israel ni Jerusalem, na mji huu haupatikani popote tena,”amesema Netanyahu

Hata hivyo, ameongeza kuwa hakuna kitu kibaya kama kuwanyima Wayahudi mji wao wa Jerusalem ambao ni halali yao.

 

Wapinzani wapigwa marufuku kushiriki uchaguzi
Gambo amtabiria makubwa Lema