Tishio la Rais, Vladmir Putin la kutumia silaha ya nyuklia nchini Ukraine iwapo uaminifu wa eneo la Urusi litatishiwa, limezua mjadala wa kina katika nchi za Magharibi.

Katika tamko lake, la mapema wiki hii Putin alisema, “Wale wanaojaribu kutudanganya na silaha za nyuklia wanapaswa kujua kwamba upepo unaweza pia kuelekea upande wao, na huu sio ujinga.”

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo hawajashawishika kuwa rais wa Urusi yuko tayari kuwa wa kwanza kufyatua silaha za nyuklia, tangu Amerika ilipoishambulia Japan mwaka 1945, ambapo bomu la atomi lililodondoshwa Hiroshima lilikuwa na kilotoni 15.

Rais wa Urusi, Vladmir Putin. Picha na New Straits Times.

Hivi karibuni, shirikika moja la Habari lilizungumza na wataalam na maafisa kadhaa kuhusu athari na hali inavyoweza kutokea, ikiwa Urusi itafanya shambulio la nyuklia na kusema huenda Moscow ikapeleka bomu moja au zaidi katika uwanja wa vita.

Wataalam hao, akiwepo Jenerali wa Kijeshi wa Pakistan, Mohamud Raja walijibu kuwa, “Hizi ni silaha ndogo ndogo, kuanzia kilo 0.3 hadi kilo 100 za nguvu za milipuko, ikilinganishwa na megatoni 1.2 za kichwa cha kimkakati kikubwa zaidi cha Amerika au bomu la megaton 58 lililojaribiwa Urusi mnamo 1961.

Wanasema katika majibu yao kuwa, “Mabomu ya wastani yameundwa ili kuwa na athari ndogo kwenye uwanja wa vita, ikilinganishwa na silaha za kimkakati za nyuklia ambazo zimeundwa kupigana na kushinda vita vya kila upande.

Rais wa Ukraine, Volodymry Zelensky. Picha na The Indian Express.

Wachambuzi hao, wanasema lengo la Urusi kutumia bomu la nyuklia la kimbinu nchini Ukraine, ni tishio na ni mbinu za kujisalimisha au kutaka meza ya mazungumzo, na kuwagawanya waungaji mkono wa nchi hiyo ya Magharibi.

Mtaalam wa kijeshi wa Mpango wa Kimataifa wa Usalama wa CSIS jijini Washington, Mark Cancian yeye anaongeza kuwa, Urusi haitaweza kutumia silaha za nyuklia katika mstari wa mbele kwani kushika maili 20 (kilomita 32), za eneo kunaweza kuhitaji mabomu 20 madogo ya nyuklia.

Cancian anafafanua kuwa, “Kutumia bomu moja pekee haitatosha, na Moscow inaweza badala yake kutuma ujumbe mzito na kuepuka hasara kubwa kwa kulipua bomu la nyuklia juu ya maji, au kulipuka moja juu juu ya Ukrainia ili kutoa mshindo wa sumakuumeme ambao ungeangusha vifaa vya kielektroniki.”

Rais wa China, Xi Jinping. Picha kwa hisani.

Ameongeza kuwa, Putin anaweza kuchagua uharibifu na kifo kushambulia kambi ya kijeshi ya Ukraine, au kupiga kituo cha mijini kama Kyiv, na kusababisha vifo vya watu wengi na pengine kuua uongozi wa kisiasa wa nchi.

Kwa upande wake Mtaalam wa zamani wa sera ya nyuklia wa White House, Jon Wolfsthal Septemba 23, 2022 aliandika kwenye Substack kuwa, “Matukio kama haya inawezekana yakaundwa ili kugawanya muungano wa NATO na makubaliano ya kimataifa dhidi ya Putin.”

Wolfsthal, aliendelea kutabanaisha katika andiko lake kuwa, “Lakini haijulikani kama Putin angefaulu, na inaweza kuonekana kuwa ni jambo la urahisi kama atachagua kukata tamaa na kusimamia matamshi yake au kama atakubali kutatua mzozo kwa njia ya mazungumzo.”

Rais wa Marekani, Joe Biden. Picha na Alex Brandon/AP

Aidha, nchi za Magharibi zimebaki na utata juu ya jinsi zinavyoweza kujibu tamko hilo la Putin kwa busara juu ya uamuzi wake wa kutaka kutumia nyuklia ikionekana kuwa zipo katika jitihada za kuchuja maneno ili kuepusha uchocheaji wa jambo hilo.

Marekani na NATO, hawataki kuonekana dhaifu mbele ya tishio la nyuklia na ndio maana wiki hii Rais Joe Biden alionesha kumbeza Putin juu ya tamko lake mbele ya mkutano jijini New York kitu kichogawa watu wanaowaza kuepusha uwezekano wa vita vya Ukraine ambayo inaweza geuka kuwa vita vya kimataifa.

Hata hivyo, Wolfsthal anasisitiza kuwa, nchi za Magharibi hazitakuwa na chaguo ila kujibu, na kwamba matamshi yao yanapaswa kutoka NATO kama tamko la pamoja na si Marekani pekee kwani watakacho muambia Putin kinapaswa kuhakikisha hakiamshi hisia za jeshi la Urusi.

Rais wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong Un. Picha na AP.

Naye, Kiongozi wa Baraza la Atlantiki, Matthew Kroenig anasema Marekani, imeweka takriban asilimia 100 ya silaha zake za nyuklia za kimbinu katika nchi za NATO na inaweza kujibu kwa mapambano dhidi ya vikosi vya Urusi na kuonesha azimio la kuikumbusha Moscow juu ya hatari ya vitendo vyake.

Kroenig anasema, “Hii inaweza pia kusababisha kulipiza kisasi kwa nyuklia kwa Urusi, na kuongeza hatari ya mabadilishano ya nyuklia na maafa zaidi ya kibinadamu na hatari nyingine ni kwamba baadhi ya wanachama wa NATO wanaweza kukataa jibu la nyuklia, wakitumikia malengo ya Putin ya kudhoofisha muungano.”

Kwa pamoja, Wataalamu wote wanasisitiza kwamba kujibu shambulio la nyuklia la Urusi kwa njia ya kawaida ni jambo la busara zaidi kuliko kutumia mbinu za kijeshi au ikiwezekana watumie njia za kidiplomasia, na kuipatia Ukraine silaha hatari zaidi kushambulia Urusi, ili kuleta ufanisi zaidi.

Silaha za nyuklia. Picha na Twitter.

Matumizi ya nyuklia ya Urusi, yanaonekana kutoungwa mkono baada ya Serikali za China na India, kutoa wito wa kufikiwa kwa makubaliano ya kumaliza vita nchini Ukraine hatua, inayoashiria kwamba washirika hao wa Urusi sasa wanaonyesha kuigeuzia mgongo sera ya uvamizi.

Awali ilidhaniwa kuwa, kauli ya Putin inaweza kutoa fursa ya kuzishawishi neno nchi hizo ambazo zilikuwa kimya kwa kutosema chochote juu ya vita hivyo, ambapo hivi karibuni Kiongozi wa Uchina Xi alikutana na Putin lakini katika hotuba yake hakutamka chochote wala kuitaja Ukraine.

Marekani, nayo inaweza kutoa ndege za NATO za Ukraine, betri za Patriot na THAAD za kuzuia mashambulizi na makombora ya masafa marefu ya ATACMS, ambayo yanaweza kutumiwa na vikosi vya Ukraine kushambulia ndani ya nchi ya Urusi.

Silaha za nyuklia ambazo zimekuwa zikioneshwa hadharani na baadhi ya mataifa yenye nguvu ulimwenguni. Picha na Reuters.

Ni busara pekee inayohitajika katika maamuzi ya nini cha kufanya ili kuepuka uwezekano wa kuibuka kwa vita nyingin ya Dunia kutokana na mataifa makubwa kuonekana wapi yameegemea zaigi kuliko kutafuta suluhu ya kudumu na kutengeneza amani kwani athari nyingi zitajielekeza kwa nchi masikini.

Ikumbukwe kuwa sehemu kubwa ya watu wanaoathirika na vita hivi ni watu wasio na hatia, ambapo kwa takwimu za hivi karibuni zinasema, takriban watoto 972 wameuawa au kujeruhiwa na ghasia tangu vita vilipoongezeka nchini Ukraine, ikiwa ni wastani wa zaidi ya watoto watano wanaouawa au kujeruhiwa kila siku.

Lakini pia, matumizi ya silaha hizi za vilipuzi yamesababisha vifo vingi vya watu na silaha huwa hazibagui raia au wapiganaji, hasa zinapotumiwa katika maeneo yenye watu wengi kama ilivyo kwa nchi ya Ukraine hasa katika maeneo yaliyoathiriwa ya Mariupol, Luhansk, Kremenchuk, na Vinnytsia, na endapo matumizi ya Nyuklia yataanza basi tutarajie madhara kwa ulimwengu zaidi ya yale yaliyotokea Hiroshima, Japan.

Makamu wa Rais athibitisha baba yake kutetea kiti cha Urais
TPA yatoa tamko ujenzi Bandari ya Bagamoyo