Taarifa kuhusu jamaa anayefahamika kwa jina la Chris Grey, ambaye anamuonekano wenye kufanana kwa kiasi kikubwa na nyota wa muziki kutoka nchini Marekani Chris Brown, zimeendelea kuenea kwa kasi kote mitandaoni.

Baada ya kutangaza kuutembelea mji wa Detroit, taarifa za Chriss zilishika hatamu kwa vyombo vya Habari ambapo ilibainishwa kuwa yeyote atakayehitaji kuonana naye, kukutana, kusalimiana na kupata picha ya pamoja, atatakiwa kumlipa Usd 1,500 kiasi ambacho ni sawa na zaidi ya 3.5 milioni za Tanzania.

Chris Grey, mtu anayetajwa kufanana na Criss Brown.

Hivi karibuni, zimesambaa picha nyingi zikimuonyesha mtu mwenye muonekano sawa na wa mwimbaji Chris brown katika miji mbali mbali, akisalimiana na kukumbatiana na watu tofauti tofauti, huku kundi kubwa la watu wakiamini ni Chris brown halisi hali ya kuwa ni kinyume.

Mpaka sasa, hakuna kauli wala ujumbe wowote kutoka kwa mwanamuziki Chris Brown kuhusu taarifa za Chris Grey, ambaye anayetamba mitandaoni na kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa kupitia muonekano wa kufanana na nyota huyo.

Kenya: Mahakama yaivutisha IEBC 'pumzi ya moto'
GGML yaungana na Serikali uboreshaji maisha ya wazee