Jeneza la Patrice Emery Lumumba, ambaye mabaki yake yalirejeshwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wiki iliyopita, limewasilishwa kwa mapumziko eneo alilozaliwa gwiji huyo la Haut-Katanga kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku wengi wakimsimulia kama shujaa wa Taifa.

Shujaa huyo wa DRC, zamani ikifahamika kama Zaire alijipatia umaarufu Juni 30, 1960 baada ya kutoa hotuba ya uhuru mbele ya Mfalme Baudouin wa Ubelgiji, akiwashutumu wakoloni kwa unyanyasaji, utumwa, kuwabagua na kudhalilisha watu wa Kongo na kumfanya kuwa shujaa wa papo hapo wa harakati za uhuru wa Afrika.

Mtendaji wa vuguvugu la kitaifa la Kongo, Joseph Anganda amesema watamkumbuka Lumumba si tu kupigania uhuru, bali kwa maono yake ya kutaka kuifanya Kongo kuwa nchi yenye umoja na nguvu akiwa kijana wa umri wa miaka 36.

“Katika hotuba yake amewahi kusema alikumbana na kashfa, matusi, vipigo ambavyo viliwalazimu kuvumilia kwani walifanyiwa hivyo asubuhi, mchana na jioni, kwa sababu walikuwa watu weusi, sasa hii kwangu naona ni mtu aliyeleta mwamko wa kisiasa Kongo,” amesema Anganda.

Baada ya kupumzika katika kijiji hicho cha Haut-Katanga, jeneza la Waziri Mkuu huyo wa kwanza wa Ubelgiji baada ya uhuru, liliendelea na safari yake ya kupitishwa maeneo mengine huku akiacha simanzi katika Kijiji hicho mahali aliponyongwa Januari 1961, miezi minne baada ya kumalizika kwa muda wake mfupi wa uongozi.

Mwili wa Lumumba uliyeyushwa kwa tindikali baada ya kuuawa, lakini afisa wa polisi wa Ubelgiji alilihifadhi jino hilo kama nyara, na baadaye mwaka 2016 Mamlaka ya Ubelgiji ilichukua mabaki ya Lumumba kutoka kwa binti yake.

Lumumba alizaliwa Julai 2, 1925 katika kijiji cha Onalua kilichopo jimbo la kati la Sankuru na wazazi wake kutoka kabila dogo la Tetela, baadaye alisomea uuguzi kisha akajiunga na shule ya posta ya utawala wa kikoloni na kuhitimu kisha kuwa karani wa huduma ya barua jiji la Stanleyville, ambalo sasa linaitwa Kisangani.

Sherehe ya mfano ya maziko ya Kitaifa ya Patrice Emery Lumumba imepangwa kufanyika jijini Kinshasa ‘zamani Leopod-ville’ Juni 30, 2022 siku ambayo ni ya Uhuru wa Taifa la Jamhuri ya Kidemokeasia ya Congo DRC, zamani ikifahamika kama Zaire.

CHADEMA 'yawakalia kooni' Mdee na wenzake
Sudan yaapa kulipiza kisasi kwa Ethiopia