Meya wa jiji la Sacramento nchini Marekani, Kevin Johnson amekumbwa na mtihani wa aina yake baada ya kupigwa usoni na sahani ya chakula wakati akizungumza na umati.

Tukio hilo limetokea juzi usiku wakati Meya huyo alipokuwa akiwasalimia watu waliokuwa wakiendelea na hafla ya uchangiaji wa hiari wa huduma za jamii. Mtu huyo aliyekuwa amebeba sahani ya chakula alimvuta Meya huyo kutoka nyuma na kumbamiza usoni.

meya-2

Kufuatia tukio hilo lililochafua hali ya hewa, Meya Johnson ambaye ni staa wa zamani wa mpira wa kikapu nchini humo aliamua kumshughulikia mshambuliaji aliyetajwa kuwa ni mwanaharakati wa jimbo hilo, Sean Thompson.

Jarida la Sacramento limeeleza kuwa Meya alimpiga ngumi kadhaa usoni na kumshambulia sehemu nyingi za mwili Thompson, kipigo kilichomsababishia majeraha makubwa.

Akizungumzia tukio hilo, Thompson alisema kuwa Meya Johnson alitumia nguvu kupita kiasi kumdhibiti kwakuwa alishonwa nyuzi 9 hospitalini na baadae kutupwa selo.

Thompson baada ya kupokea kipigo

Thompson baada ya kupokea kipigo

Alisema chanzo cha kumshambulia Meya ni kutokana na kukasirishwa na kitendo chake cha kutojikita katika kusaidia wenye mahitaji na badala yake anaonekana kutumia nguvu nyingi kwa timu ya kikapu ya jiji hilo.

Msemaji wa Meya, Bryce Heinlein pamoja na Jeshi la Polisi la jiji hilo walithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa kabla ya tukio hilo wawili hao walionekana kuzozana majira ya saa 12 jioni ya siku hiyo.

“Meya alimpiga mtuhumiwa baada ya kushambuliwa kwanza,” alisema Heinlein.

Picha: Waziri Mkuu awasili Mafia kuanza ziara Mkoani Pwani
Video: DC Mjema - Serikali ipo macho, Atoa mikakati kupambana na uhalifu Ilala