Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umeshiriki katika Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Kihesa Kilolo mkoani Iringa.

Maonesho hayo, yalifungwa na Mgeni Rasmi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo na Wananchi.

NSSF, ilitumia maonesho haya kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kuandikisha wanachama, kusikiliza na kutatua kero za wanachama.

Mgeni Rasmi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.
Viongozi EAC waratibu mazungumzo ya amani
Mawaziri watoa maagizo ajali ya Ndege