Uvumi wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi kati ya mwimbaji Rihanna na muigizaji tajiri, Leonardo DiCaprio umepewa sura mpya na mapaparazi waliokuwa kazini kwenye club moja ya usiku jijini Paris, Ufaransa.

Picha zilizonaswa na lens ya paparazi hao zimewaonesha wawili hao wakiwa karibu na baadae kupeana busu la huba huku Rihanna akionekana kuwa katikati ya bwawa la mapenzi lenye kina cha bonde la Ziwa Tanganyika.

Rihanna na DiCaprio

Hata hivyo, wawakilishi wa DiCaprio walimtetea na kudai kuwa picha hiyo ilinaswa wakati wawili hao walipokuwa karibu na kugusana bila kukusudia wakati wanacheza.

Rihanna na DiCaprio2

Mwenye macho haambiwi tazama.!

Hello ya Adele yavunja rekodi nyingine ya Dunia YouTube
Nyota Wa Kikapu Wa Malawi Kuzikabili Timu Za Dar