Spika wa Bunge, Job Ndugai ameambatana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid pamoja na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai wamefika nyumbani kwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa kutoa pole kwa mjane Mama Anna Mkapa Masaki, Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge, Job Ndugai akisaini kitabu cha maombolezo
Spika wa Bunge, Job Ndugai na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid wakitoa pole kwa mjane Mama Anna Makapa
Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid, Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu nchemba baada ya kutoka ndani kwa Rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi (katikati), amefika nyumbani kwa hayati, Benjamin Mkapa Rais Mstaafu awamu ya tatu kutoa pole kwa Mama Anna Mkapa, nyumbani kwao Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi,akisaini Kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Benjamin Mkapa Rais Mstaafu awamu ya tatu, kulia ni mwanasheria wa Benki hiyo, Mystica Ngongi na  kushoto ni Kaimu Meneja Mwandamizi kitengo cha uhusino na mahusiano wa Benki hiyo Chichi Banda. 
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa pole kwa mke wa marehemu wengine wa pili kushoto mwanasheria wa Benki hiyo Mystica Ngongi wa kwanza kushoto Kaimu Menej Mwandamizi kitengo cha uhusino na mahusiano wa Benki hiyo Chichi Banda. 

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 28, 2020
Polisi Tanzania kusajili wazawa