Klabu ya Manchester United imempiga marufuku kiungo wake Paul Pogba kucheza mchezo wa kikapu kwa madai kuwa mchezo huo unachangia kiungo huyo kupata maumivu ya misuli ya mapaja.

Pogba ambaye kwa sasa yupo nje ya uwanja akisumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja aliyopata katika mechi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Basel mapema mwezi jana ni mpenzi wa mchezo wa kikapu.

Awali kocha wa Man Utd Jose Mourinho alisema kuwa Pogba hatarajii kurejea mapema uwanjani na ingemchukua wiki 6 lakini tayari mchezaji huyo ameanza kufanya mazoezi hali inyoonyesha maendeleo mazuri ya afya yake.

Image result for paul pogba play basketball

Image result for paul pogba play basketball

 

 

Video: Itazame ngoma mpya ya Aslay 'Natamba'
Vanessa ‘ateka’ tuzo za kimataifa, fanya haya umpe ushindi