Masaa kadhaa baada ya kusambaa kwa barua ya Spika wa Bunge ikitaja Mabadiliko madogo ya Kamati za kudumu za Bunge, Mbunge wa Kuteuliwa Humphrey Polepole kupitia ukurasa wake wa Instagram amemjibu Kiongozi huyo.

Katika maelezo yake Polepole amesema ameyapokea kwa furaha na shauku kwa kuwa yanamuanzishia safari nyingine ya Shule ya uongozi na mafunzo kwa Vitendo.

Amesema baada ya miezi 9 ya kuhudumu katika dhamana ya uenyekiti wa kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa na sasa kuwa mjumbe katika Kamati ya Sheria Ndogo anaendelea kulituikia Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali kwa ujumla.

Katika mitandao yake ya kijamii mwanachama huyo wa Chama Cha Mapinduzi huweka mada mbalimbali zenye Jina la Shule ya uongozi akiwa na nia ya kuwaelimisha jamii juu ya uongozi kwa ngazi tofauti.

Waziri Ummy asitisha mfumo wa kielektroniki wa maegesho ya magari
Polepole avuliwa uongozi