Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini leo limetoa tamko kuhusu tukio la kupotea kwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bernard Saanane.

Saanane alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Novemba 18 mwaka huu ambapo familia, uongozi wa Chadema na marafiki walieleza kuwa hawafahamu alipokwenda na kwamba simu zake zote zilikuwa hazipatikani.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kamishna Robert Boaz amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini alipo.

“Tunachunguza taarifa za kupotea mwananchi mwenzetu, Benard Saanane ambaye taarifa zake zilifikishwa Polisi tarehe 5 mwezi wa 12. Tunaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuweza kujua huyu mtu yuko wapi, alisema Kamishna Boaz.

Aidha, aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na jinsi walivyoweza kutoa taarifa mbalimbali kuhusu kupotea kwa Sanaanane.

Aliahidi kuwa Jeshi hilo litazifanyia kazi taarifa zote wanazozipokea ili waweze kufahamu alipo na nini kilichomsibu.

Msongo Wa Mawazo Wamvuruga Alexis Sanchez
Nay wa Mitego achukua hatua kumsaidia Chid Benz kuachana na ‘Unga’