Jumla ya Polisi 12 wa nchini Ghana wameruhiwa huki wakiwakamata watu 29 waliofanya ghasia wakati wakitawanya  maandamano ya Raia wanaopinga kupanda kwa gharama za maisha jijini Accra.

Waandamanaji hao, walikuwa waliandamana katika mitaa ya mji huo mkuu wa Ghana huku wakiwa wameshikilia mabango yaliyoandikwa “Mheshimiwa Rais, tulikosea wapi?, Gharama kubwa ya maisha itatuua”.

Tukio hilo, linalodaiwa kutokea alasiri ya Juni 28, 2022 zaidi ya waandamanaji 100 walijaribu kukengeuka kutoka kwa njia rasmi ya maandamano hayo, kwabkuyafanya yaonekane kuwa na dhamira ya vitendo vya uhalifu na jinai.

Hatua hiyo, ilisababisha Maafisa wa Polisi kuwawekea vizuizi, kitu kilichosababisha waandamanaji kuwarushia mawe na Polisi walijibu kwa kutumia vilipuzi vya gesi ya kutoa machozi ili kuutawanya umati huo na kupelekea baadhi yao kujeruhiwa.

“Ni aibu iliyoje, tulikuwepo kuwalinda ili mfikishe ujumbe na sisi kuhakikisha usalama wenu, lakini mnaturushia mawe na kutujeruhi, maafisa wetu 12 wamejeruhiwa,” Polisi waliandika kupitia ukurasa wao wa mtandao.

Hata hivyo, baadaye Polisi ilithibitisha kukamatwa kwa waandamanaji hao 29 na kusema, “waandaaji wa maandamano hayo watakamatwa na kufikishwa mbele ya Mahakama ya sheria kwa kushambulia Polisi na kuharibu mali ya umma”.

Kwa miezi kadhaa, wananchi wengi wa Ghana wamekuwa wakiandamana kupinga ongezeko la bei ya chakula na mafuta, hivyo kumshinikiza Rais Nana Akufo-Addo kujiuzulu.

Janga la Uviko-19 na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, limesababisha kuongezeka kwa mfumuko wa bei hadi zaidi ya asilimia 27 kwa mwezi juni, kiwango ambacho kinatajwa kuwa ni cha juu zaidi kwa miongo miwili katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

“Tunateseka na kibaya zaidi hatujui hatma yetu na Viongozi wapo kimya hii ni mbaya sana, hatuwezi hata kumudu milo mitatu kwa siku na bei za usafiri na vyakula ni kubwa mno,” alilalama muandamanaji Baba Musah mkarabati wa simu mbovu za mkononi.

Viongozi wengi wa upinzani nchini humo walikuwepo kwenye maandamano hayo, yaliyoandaliwa na washawishi toka kikundi cha Arise kilichopo jijini Accra, Ghana.

Gabriel Jesus: Chanzo ni msichana aliyenidharau
Fiston Mayele ampongeza George Mpole