Maafisa wa Jeshi la Polisi Minnesota nchini Marekani wameripotiwa kususia kulinda mechi kati ya Dallas Wings na Lynx baada ya wachezaji na baadhi ya mashabiki kuvaa fulana zenye maandishi mbalimbali pamoja na picha za watu weusi wawili waliouawa hivi karibuni na polisi wazungu.

Maandishi ya fulana hizo yalilenga katika kupeleka jumbe za kupinga mauaji hayo zinazotokana na harakati zilizoanzishwa hivi karibuni zinazotetea uhai wao ‘Black Lives Matter’.

Mkuu wa Jeshil la Polisi katika jimbo la Minnesota, Lt. Bob Kroll amesema kuwa anawapongeza maafisa hao wa polisi kwa kitendo walichokifanya. Alisema anaamini hata askari wenzao wanaweza kuamua kususia ulinzi sehemu nyingine endapo watu wanaowalinda watakuwa na fulana zenye jumbe hizo zinazoliponda jeshi hilo.

“Kama wachezaji wataendelea kufanya hivyo, maafisa wote wanaweza kususia kufanya kazi huko, na mimi nawasifu kwa hilo,” alisema Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Minnesota.

Watu weusi wamekuwa wakionesha hasira zao kwa namna mbalimbali dhidi ya vitendo vya mauji yaliyofanywa na maafisa wa polisi wa kizungu dhidi ya watu wawili weusi katika matukio tofauti, baada ya kuwatia nguvuni. Matukio hayo yalirekodiwa na kusambazwa katika vipande vya video.

Rashid Mandawa,Cassian Ponera Wasajiliwa Mtibwa Sugar
Jeshi Kuanza Mafunzo ya Kupambana na Ugaidi