Maafisa ununuzi na Ugavi wote wa serikali na wasio wa serikali wametakiwa kujisajili katika kanzidata ya PSPTB ili kuhakikisha Kazi za ununuzi wa umma zinaharakishwa na kutochelewesha miradi ya serikali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi PSPTB,  Godfred Mbanyi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa ofisi za PSPTB.

Amesema, “Wale wote wanaofanya kazi za ununuzi we ni wa serikali au shirika binafsi Nchini ili maradi unahusika na ununuzi wa umma basi wahakikishe wamesajiliwa na Bodi ya Ununuzi na Ugavi ili mfumo mpya utakapoanza kufanya kazi maafisa ununuzi wote waweze kuanza kazi kwa kishindo na kuepusha kuchelewesha shughuli za umma,”

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi PSPTB,  Godfred Mbanyi.

Mbanyi amebainisha kuwa Serikali kwa sasa inajenga mfumo mpya wa ununuzi wa umma ambao unajengwa na Watanzania wenyewe tofauti na mfumo wa awali wa TANePS ili kupunguza changamoto ambazo zilikuwa zinajitokeza katika mfumo wa awali wa ununuzi.

Amesema changamoto kubwa iliyokuwepo hapo awali ni kuwa Mtaalamu yoyote alikuwa anaweza kufanya ununuzi katika mfumo huo hata kama alikua hahusiki na bodi na wala hajasajiliwa hali iliyokuwa inasababisha madhaifu mengi ya kiununuzi na kukuta mapungufu wakati wa ukaguzi wa Mdhibiti wa hesabu za serikali.

“Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali alikua akifanya Ukaguzi katika mashirika yanayohusu ununuzi na Ugavi anakuta kuna madhaifu mengi katika ununuzi wa umma na mashirika nunuzi ambapo wagtu walionekana wamenunua visivyoonekana, hivyo kwa mfumo huu mpya mtu yoyote hatapiga hatua yoyote katika mfumo kabla ya kuulizwa namba yake ya Bodi, ambayo kwenye kanzidata inafahamika. Usipoweka namba ya usajili ina maana mfumo utakataa kukushughulikia,” amesema Mbanye.

“Hii ina maana kwamba mfumo mpya umeunganishwa na kanzidata ya PSPTB, ambapo mtu alimtaka kuitangaza zabuni akaingiza namba ya usajili ya PSPTB, na atarahisisha kazi zake za manunuzi,” ameongeza.

Aidha ameongeza kuwa hivi karibuni kuna Ukaguzi utakaofanyika katika mashirika yote ya umma ili kuhakikisha maafisa wote wanaohusika na ununuzi wa Umma wana sifa zote zinazotakiwa na Bodi.

“Ukaguzi huu utafanyika kuanzia Septemba 13, 2022 na utaanza na mashirika makubwa ya Umma ambapo tutakagua mnunuzi aliesomea, aliefanya mitihani yote, aliesajiliwa na bodi ya Ununuzi na Ugavi, kiufupio sifa zote wanazifahamu na ni lazima wawe nazo zote.” Alimaliza kueleza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi PSPTB,  Godfred Mbanyi.

Kwa Mujibu wa kifungu cha 46 cha Sheria Namba 23 ya mwaka 2007, ni kosa kisheria kwa mtu yoyote kujishughulisha na shughuli za ununuzi wa Umma na Ugavi bila kusajiliwa na bodi ya PSPTB.

Tanzania na Qatar 'zabadilishana' mikakati
Waziri Mkuu aombwa kujiuzulu kwa 'kukata mauno' hadharani