Rais wa Urusi, Vladmir Putin ameagiza kufukuzwa kazi kwa wamarekani 755 waliokuwa wakifanya kazi katika ubalozi wa Marekani nchini Urusi kufuatia hatua iliyochukuliwa na Marekani ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo.

Hatua hiyo mekuja mara baada ya bunge la Marekani kupitisha sheria ya kuiwekea vikwazo Urusi mara baada ya kubainika kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani uliofanyika mwaka jana.

Putin amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuchukua hatua zingine kali zaidi za kuiadhibu Marekani kufuatia hatua waliyoifikia, huku akitahadharisha kuwa uhusiano kati ya nchi hizo kuwa utadorola.

Kwa upande wake Marekani imesema kuwa imesikitishwa na hatua zilizochukuliwa na Urusi hivyo inaangalia namna ya kuweza kujibu mapigo hayo ingawa yanazorotesha uhusiano mzuri uliokuwepo.

Hata hivyo, Mashirika ya Kijasusi ya Marekani yanaamini kuwa Urusi iliingilia Uchaguzi Mkuu wa Urais wa mwaka 2016 kwa lengo la kumsaidia Donald Trump kupata ushindi kitu ambacho Urusi imekanusha vikali kuingilia uchaguzi huo.

Mndeme ampa tano Mavunde, amtaka aendeleze kasi ile ile
Jeshi la zimamoto nchini kushirikiana na Kuwait kukabiliana na majanga ya moto