Mkongwe wa muziki  nchini Marekani R Kelly ameshtakiwa kwa makosa 11 ya unyanyasaji wa kingono kwa mabinti waliokuwa chini na umri wa miaka 16.

Kwamujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, Mahakama imeripotiwa kuwa vitendo hivyo vilifanywa kwa watoto wa umri kati ya miaka 13 na 16 na ikiwa itathibitika kufanya kitendo hicho atakabiliwa na adhabu kali kuliko adhabu nyingine anazokabiliwa nazo.

Mwanzoni mwa mwaka huu kellz alikabiliwa na mashtaka kumi ya unyanyasaji wa kingono, alikana kuhusika na vitendo hivyo na akaachiwa kwa dhamana.

Hata hivyo R kelly anaimani kubwa ya ushindi dhidi ya mashtaka yake kumi yanayo mkabili, huku kesi zake kuanza kusikilizwa hivi karibuni mjini Chicago.

Licha ya kesi ya unyanyasai wa kingono msanii huyo anakabiliwa na kesi ya ukwepaji kodi na kusafirisha wanawake kwaajili ya kufanyanao ngono.

 

 

Washtakiwa wa mauaji Uganda kujipangia Adhabu
Museveni amruhusu mkuu wa MTN kurejea nchini humo

Comments

comments