Rais wa Zambia,  Edga Lungu ametoa amri ya kila mwananchi wa nchi hiyo ni lazima afanyiwe vipimo vya ugonjwa ukimwi ili kuweza kujua ni jinsi gani anaweza kusaidiwa asiweze kusambaza maambukizi kwa wengine.

Rais huyo amefikia hatua hiyo mara baada ya nchi hiyo kuwa ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa huo kusini mwa bara la Afrika ikiwa na asilimia 11.6 huku watu walio na umri wa miaka kuanzia 15 mpaka 49 wakiishi na virusi vya ukimwi.

Aidha, Lungu ameongeza kuwa kupimwa ukimwi na kupewa ushauri pamoja na matibabu si jambo hiari bali ni lazima kwakuwa zoezi hilo limelenga kuweza kupunguza maambukizo ya ugonjwa huo nchimi humo.

Lissu aitunishia misuli mahakama, asema vishungi sio bangi
Nchemba awaonya jamii ya wafugaji wasiopeleka watoto shule