Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza matumaini yake kuwa, iwapo dhana ya Uchumi wa Buluu itaeleweka vyema kutakuwa na nafasi nzuri ya kurekebisha na kuboresha sheria na taratibu za Mahakama katika safari ya kuujenga uchumi wa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria uliofanyika huko katika viwanja vya Nyerere Squire, Jijini Dodoma uliokwenda sambamba na uzinduzi wa Nembo pamoja na Bendera ya Mahakama.

Alieleza kwamba kwa lugha nyengine sheria na taratibu za Mahakama zilizopo lazima ziendane na mipango iliyopo ya Serikali yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi kupitia Uchumi wa Buluu.

Alisisitiza kwamba Zanzibar haikujaaliwa ardhi kubwa kwani ni nchi ya visiwa ambapo idadi ya watu wake imeongezeka mara tano katika kipindi cha miaka 56 ambapo mwaka 1964 Wazanzibari walikuwa laki 3 tu ambapo hivi sasa wapo takriban 1.6.

Katika hotuba hiyo Rais Dk. Mwinyi alitoa wito kwa Wanasheria na wataalamu wa sheria, viongozi wa Mahkama na watumishi wa sekta za sheria kuielewa na kuifanyia kazi mipango mikuu ya uchumi wa Tanzania na kuwa huru kutoa ushauri wa kisheria Serikalini kwa lengo la kuifanikisha.

Sugu anarudi kwa kishindo
Haya ndo madhara ya ngono ya mdomo