Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amewasili nchini na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais Ndayishimiye amewasili mapema leo Oktoba 22, 2021, jijini Dodoma, kwa ajili ya ziara yake ya kitaifa ya siku tatu ambapo atakwenda pia Zanzibar kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Hussein Mwinyi.

Pamoja na mambo mengine, Rais Ndayishimiye anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha mbolea, kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na kukagua ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.

Pia, Rais Ndayishimiye atatembelea Bandari Kavu ya Kwala inayojengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania katika eneo hilo.

Madeni kwa Serikali yaikwamisha PSSSF
Wivu wa Mapenzi wamponza mtoto wa Floyd Mayweather