Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemkabidhi Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Dkt. Kiva Mvungi cheti kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kupitia Mfuko wa UKIMWI wa Taifa (AIDS Trust Fund).

Rais Samia akimkabidhi Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited, Dkt. Kiva Mvungi cheti kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

GGML imepokea zawadi hiyo, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo kitaifa yamefanyika Disemba 1, 2022 Mkoani Lindi huku kampuni hiyo ikiahidi kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kupitia Kampeni ya Kili Challenge.

Kampeni hiyo, iliyozinduliwa na GGML miaka 20 iliyopita ikilenga kuongeza uelewa pamoja na kukusanya fedha za mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI.

Roberto Martínez abwaga manyanga
Wizi wa pesa shambani: Rais atakiwa kujiuzulu