Uongozi wa Klabu ya Us Monastir, umesema kuwa wapinzani wao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Young Africans, ni watu ambao hawana ungwana katika Soka, hasa baada ya tukio la viongozi wa Club African, kumwagiwa maji walipokuja Tanzania kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza Hatua ya Mtoano.

Miamba hiyo inatarajiwa kuanza kukutana mwishoni mwa juma hili (Jumapili Februari 12), mjini Tunis Tunisia kabla ya kukutana tena jijini Dar es salaam Machi 19.

Rais wa Klabu ya US Monastir Harnart Mozant amesema: “Young Africans ni timu ndogo sana hapa Afrika, ila wanayo matukio mengi katika michezo michache ya kimataifa na matukio yao sio ya kiungwana katika soka, US Monestir tunaamini tutakapokwenda Tanzania watatufanyia kama walivyowafanyia wenzetu wa Club African,”

“Us Monestir, tuna uzoefu wa mashindano ya kimataifa hivyo matukio kama yale ambayo Young Africans waliyafanya, kwetu ni kawaida mno kukutana nayo.”

Katika hatua nyingine Rais huyo wa Monestir, amesema wanaimani Young Africans, haina uwezo wa kuchukua hata alama moja watakapokutan nao iwe nyumbani au ugenini.

Amesema waliitazama Young Africans ilipocheza dhidi ya Club Africain, ambayo ipo katika hati hati ya kushuka daraja, hivyo hawana papara zaidi wa kuwasubiri wafike Tunisia ili wakipige Jumapili.

Kwa sasa US Monestir ipo nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Tunisia, katika Kundi B ikitanguliwa na Ben Guerdane.

TP Mazembe waishughulisha Young Africans
25 kuifuata US Monastir Tunis-Tunisia