RAIS wa zamani wa mpito wa Bolivia Jeanine Anez amefanya jaribio la kujiua akiwa jela siku moja baada yakufunguliwa mashtaka ya “mauaji ya halaiki” kutokana na vifo vya waandamanaji vilivyotokea mwaka 2019.

Mmoja ya mawakili wa Anez, Jorge Valda, amesema kiongozi huyo wa zamani ambaye amefadhaishwa na tuhuma zinazomkabili alijaribu kuondoa uhai wake lakini jaribio hilo limeshindwa.

Anez,  anashikiliwa  tangu mwezi Machi mwaka huu kwa madai ya kufanya mapinduzi dhidi ya mtangulizi wake na Rais wa zamani wa Bolivia, Evo Morales.

Mwanasiasa huyo mwenye sera za kihafidhina aliingia madarakani kama kiongozi wa mpito mwaka 2019 baada ya Morales kujiuzulu na kuikimbia nchi hiyo lakini wapinzani wanasema hatua yake ya kuchukua madaraka ilikuwa sawa na mapinduzi.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 23, 2021
Rais Samia: Wanamichezo mkapate chanjo ya Corona