Rais wa Zambia Haikande Hichilema ametumia ndege ya abiria kwenda nchini Marekani kwenye mkutano wa umoja wa Mataifa (UN), badala ya kutumia ndege binafsi ya rais huku akiwa na msafara wa watu watatu.

Hichilema amesafiri kwa kutumia shirika la ndege la Qatar kuelekea jijini New York, Maerekani kushiriki mkutano wa 76 wa Baraza kuu la umoja wa Mataifa unaotarajiwa kufanyika Septemba 23 mwaka huu.

Hichilema amesema mpangilio wa safari yake umelenga kubana matumizi.

“Tunakwenda New York kushiriki Mkutano Mkuu wa UN, tunakwenda kushirikiana na wadau mbalimbali na muhimu kwa faida ya nchi yetu. Tumekwenda wajumbe wachache ili kazi hii iwe na tija na gharama nafuu zaidi kwa taifa letu,” amesema Hichilema.  

Shahidi kesi ndogo ya mbowe atoa ushahii
Manny Pacquiao atangaza kugombea Urais