Muigizaji wa filamu za Kitanzania (Bongo Movies), Rammy Galis ameielezea furaha aliyonayo baada ya kupata nafasi ya kufanya filamu na waigizaji wakubwa barani afrika, Aki na Ukwa.

Muigizaji huyo amesema filamu hiyo ambayo inaitwa ‘Welcome to Lagos’ itaanza kurekodiwa mwezi Disemba mwaka huu nchini Nigeria.

Akizungumza na ‘BongoDotHome’ ya 100.5 Times FM, Ramy amesema hii itakuwa nafasi nzuri ya kuweka tasnia ya filamu nchini kwenye ramani ya kimataifa.

“Nina project na Aki na Ukwa wale tumezoe kuwaona kama vi-emoro na script ipo kwenye E-mail (barua pepe),” alisema Rammy na kuongeza, “naenda kushoot Disemba movie inaitwa ‘Welcome to Logos’.”

Muigizaji huyo ambaye hivi karibuni ameitambulisha filamu yake mpya ya ‘Red Flag’ iliyosimamiwa na watayarishaji kutoka Nollywood amesema filamu hiyo inahusu mahusiano na vioja vya kufurahisha.

“Filamu inahusu mtu ambaye sio raia wa Nigeria ambaye anaenda Nigeria kwa Girlfriend wangu, kwa hiyo nafikia kwenye nyumba yake halafu Aki na Ukwa ni wadogo zake,” alisema.

“Kwa hiyo wanakuwa shemeji zangu, mimi nakuwa kama king’asti, sina hela, kwahiyo yule msichana akienda kazini nakuwa napambana na hao akina Aki na Ukwa ambao hawanipendi wananifanyia vituko,” amesema Ramy Galis.

Rais Karia apongeza baraza jipya la mawaziri
N'Golo Kante aondoka kambini Ufaransa