Rapa wa Marekani mwenye asili ya Ujerumani, Deso Dogg aliyejiunga na Kundi la kigaidi la ISIS ameripotiwa kuuwa nchini Syria.
Taarifa kutoka Pentagon zimeeleza kuwa rapa huyo ambaye jina lake la kuzaliwa nai Denis Cuspert, aliyejibadili jina na kuwa Abu Talha al – Almani aliuawa Octoba 16 katika shambulizi la ndege lilifanywa na majeshi ya Marekani nchini Syria kulenga kundi la ISIS.
Deso Dogg aliwahi kufanya ziara ya kimuziki na DMX lakini aliamua kuachana na muziki mwaka 2012 na kujiunga na kundi la ISIS.