Mkurugenzi mkuu wa maandalizi ya michuano ya tenisi huko Indian Wells, Raymond Moore amejiuzulu baada ya matamshi yake yaliozua utata kuhusu wanawake katika mchezo huo.

Moore mwenye umri wa miaka 69, alisema mchezo wa tenisi kwa wanawake unategemea sana wanaume, maoni yalioelezewa kuwa ni ya ubaguzi wa jinsia na muungano wa tenisi nchini Marekani USTA.

Mchezaji nambari moja duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams alisema kuwa matamshi ya Moore yalimkera na hayakua na ukweli wowote.

Lakini kwa upande Novak Djokovic alidai kuwa ziara yake inafaa kupigania wanaume wapewe fedha zaidi.

Moore alisema wachezaji wanawake wanafaa kuwapigia magoti wanaume kama Roger Federer na Rafael Nadal.

Gwiji wa mchezo huo Martina Navratilova alisema kwamba matamshi ya Moore yanachukiza sana, akiongezea kuwa wachezaji wanawake huenda wakasusia michuano ya Indian Wells iwapo Moore ataendelea kuwa katika nafasi yake ya ukuu wa maandalizi.

Djokovic ambaye alishinda taji la BNP la Paribas Open huko India Wells mwishoni mwa juma lililopita aliyaelezea matamshi ya Moore kama yasio sawa.

Lakini raia huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 28 alihoji kwamba wanaume wanafaa kupewa fedha zaidi kwa sababu watu wengi huangalia michezo yao.

Petr Cech Mchezaji Bora wa Jamuhuri ya Czech
Habari Mpasuko: Chadema yashinda 'Umeya' wa Dar