Klabu za Chelsea na Manchester United zinatarajiwa kuingia katika vita ya kuwawania wachezaji wawili kutoka Real Madrid Raphael Varane na James Rodriguez utakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Jose Mourinho ambaye anapigiwa upatu wa kupewa jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Man Utd, amewaweka wawili hao katika orodha ya wachezaji ambao anatarajiwa kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Mourinho anaamini kama atakabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi cha Man Utd mwishoni mwa msimu huu, haitokua kazi kubwa kuwasajili wachezaji hao wawili kutokana na kuamini kwamba mazingira aliyojiwekea wakati akiwa Real Madrid yatamsaidia kuwapata kirahisi.

Varane alisajiliwa na Mourinho mwaka 2011 akitokea nchini kwao Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Lens na mara kwa mara alipewa nafasi kwenye kikosi cha Real Madrid, hadi kufikia hatua ya kujihakikishia ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza kila juma.

Lakini James Rodriguez, hakusajiliwa na meneja huyo kutoka nchini Ureno, na jambo hilo halitomkwamisha Mourinho kuamini atamkosa katika mikakati yake, endapo akabidhiwa jukumu la kukiongoza kikosi cha Man Utd.

Kwa upande wa Chelsea, wanaamini ujio wa meneja wao mpya kutoka nchini Italia Antonio Conte utakua kivutio kwa wachezaji wengi barani Ulaya wakiwepo Raphael Varane na James Rodriguez.

Wachzaji hao wameanza kutajwa hawatokuwepo katika mipango ya meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane ambaye amejipanga kufanya usajili wa wachezaji ambao watakiwezesha kikosi chake kupambana vilivyo msimu ujao wa ligi ya nchini Hispania.

Waingereza Wamkebehi Neymar, Wamshindanisha Na Njonjo
Marcelo Bielsa Kupambanishwa Na Brendan Rodgers Swansea City