Kiungo mshambuliaji wa Real Madrid Lucas Vázquez Iglesias, amekubalia kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Uongozi wa klabu hiyo inayoongoza msimamo wa ligi ya nchini Hispania umethibitisha na kutangaza taarifa hizo katika vyombo vya habari.

“Vázquez amekubali kusaini mkataba mpya, ambao utamuwezesha kuendelea kuwepo klabuni hapa hadi Juni 30, 2021.

“Siku ya Alkhamis saa 7:30 mchana, Lucas Vázquez atakamilisha mpango huu na atazungumza na vyombo vya habari ili kueleza hisia zake.” Ilieleza taarifa ya Real Madrid.

Real Madrid ilimsajili Vázquez mwaka 2007, akitokea katika kituo cha kulea na kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana cha Ural, na tangu Zidane alipokabidhiwa majukumu ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi, amekua akipata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

Aliwahi kusajiliwa kwa mkopo kwenye klabu ya Espanyol katika msimu wa 2014-15 na alicheza michezo 33 na kufunga mabao matatu.

Msimu uliopita alirejea Santiago Bernabéu na mpaka sasa ameshacheza michezo 33 na kufunga mabao manne.

NSSF yakiri ufisadi mzito ujenzi wa mji mpya wa trilioni 1.4
Jackson Martinez Kurejeshwa Ulaya